Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa matendo yote huzingatiwa nia, na hukumu hii ni ya ujumla katika amali zote, kwanzia ibada na miamala, atakaye kusudia kupata masilahi katika amali yake hatopata zaidi ya masilahi na wala hatopata thawabu, na atakayekusudia katika amali yake kujiweka karibu na Allah Mtukufu, atapata thawabu na malipo kupitia amali yake hata kama litakuwa ni jambo la kawaida, kama kula na kunywa. Kisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akapiga mfano wa kuweka wazi namna gani nia inaathiri matendo pamoja nakuwa huonekana yote yako sawa katika muonekano wa juu, akaweka wazi kuwa atakayekusudia katika kuhama kwake na kuacha nchi yake ni kutafuta radhi za Mola wake, basi kuhama kwake kutakuwa ni kwa kisheria na kunakubalika, atalipwa kwa sababu ya ukweli wa nia yake, na atakayekusudia kwa kuhama kwake ni kupata masilahi ya kidunia, kama mali, au cheo, au mke, basi hatopata kwa kuhama kwake huko zaidi ya manufaa aliyoyakusudia, na wala hatokuwa na fungu la malipo na thawabu.