Aliwauliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake Maswahaba zake: Je, nikuelezeni lililo bora kuliko kuzidisha ibada za sunna kama swaumu na swala na sadaka? Wakasema: Ndio. Akasema: Ni kuwapatanisha waliogombana kwani ugomvi huleta mfarakano na kujitenga na kuchukiana na kupeana migongo kati ya watu, kwani yanayoambatana na kuharibika kwa mahusiano baina ya watu miongoni mwa chuki ndio jambo ambalo katika tabia zake huangamiza na kuing'oa dini na dunia kama wembe unavyong'oa nywele.