Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake baadhi ya neema za peponi, nakwamba muumini ndani ya pepo atakuwa na hema pana kwa ndani, lilitokana na madini ya lulu yenye kung'aa, upana wake na urefu wake kuelekea juu ni maili sitini, katika kila mahali na kila kona katika kona zake nne kuna wake, na wote hawaonani, muumini atakuwa akiwazungukia.