Amebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Moto umezungukwa na kuzingirwa na mambo ambayo nafsi inayatamani, kama kufanya maharamisho au uzembe katika mambo ya wajibu; Atakayeendekeza matamanio ya nafsi yake katika hilo atastahiki moto, nakuwa Pepo imezungukwa na kuzingirwa na mambo ambayo yanachukiwa na nafsi; kama kudumu katika maamrisho na kuacha maharamisho na kuvumilia juu ya hilo, atakapovumilia na akapigana vita na nafsi yake juu ya hilo atastahiki kuingia Peponi.