Anatahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu aina mbili za watu ambao ni katika watu wa motoni, hajawaona na hawakuwepo katika zama zake, bali aina hizo zitatokea baada yake: Aina ya kwanza: Ni watu walio na Mijeledi mirefu kama mikia ya Ng'ombe, wakiwapiga watu kwayo, nao ni Polisi na wasaidizi wa viongozi wasiowaadilifu, wanaowapiga watu bila hatia. Aina ya pili: Ni wanawake waliovua vazi la heshima na haya walizoumbiwa nazo mwanamke kawaida. Na sifa zao: Kwa muonekano wamevaa, na kwa uhalisia wako uchi; kwa sababu wamevaa nguo nyepesi zinazoonyesha ngozi, na wamefunika sehemu ndogo tu katika mili yao na wameacha wazi sehemu nyingine; kwa ajili ya kuonyesha urembo wao, nyoyo za wanaume zinavutika kwao kwa sababu ya mavazi yao, na kutembea kwao kwa maringo, wakinengua mabega yao, na wanawavutia wanawake wengine pia katika kupinda kimaadili, na kupotea waliko tumbukia ndani yake, Na miongoni mwa sifa zao pia: Vichwa vyao ni mfano wa nundu za Ngamia zilizopinda, utawakuta wakiipa kipaumbele mionekano ya vichwa vyao, wakiikuza kwa kukunja misuko na mfano wake, Na kufananishwa na nundu za Ngamia, ni kwa sababu kuinuka kwa nywele zao na misuko yao juu ya vichwa vyao, na kuzikunja kwao kwa sababu ya misuko mpaka zinalalia upande mmoja wa kichwa kama inavyolalia upande mmoja nundu ya Ngamia. Mwanamke atakayekuwa na sifa hizi, atakuwa na ahadi hii kali ya kutoingia peponi na wala hatopata harufu yake na wala hatoikaribia, na harufu ya pepo hupatikana na hunuswa kutoka masafa ya mbali.