Alieleza Mtume rehema amani ziwe juu yake kuwa kila Muumini atasimama mbele ya Mwenyezi Mungu Siku ya Kiyama peke yake, na kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu atazungumza naye bila ya muwakilishi, na hakuna mkalimani baina yao wa kutafsiri maneno, hivyo atatazama kulia na kushoto kutokana na hofu kali, labda atapata njia ya kwenda ili aweze kuokolewa na moto uliombele yake. Akitazama upande ulioko kuliani kwake hatoona isipokuwa yale aliyoyatanguliza katika matendo mema, na akitazama kushotoni kwake hatoona isipokuwa yale aliyoyatanguliza katika matendo mabaya, na akitazama mbele yake hatoona isipokuwa moto, na hatoweza kuukwepa, kwani hakuna budi ni lazima apite juu daraja (Swirat). Kisha akasema rehema na amani ziwe juu yake: Wekeni kinga kati yenu na moto, kama kutoa sadaka na matendo mema, walau kwa kitu kidogo kama nusu ya tende.