explain-icon

Ufafanuzi

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa wale wenye kuwahurumia wenzao huwahurumia Rahman -Mwingi wa rehema- kwa huruma yake iliyokienea kila kitu; Yakiwa ni malipo sawa na matendo yao. Kisha akaamrisha -Rehema na amani ziwe juu yake-kuwahurumia wote walioko ardhini kwanzia binadamu au wanyama au ndege, au wengineo katika aina ya viumbe mbali mbali, na malipo ya hilo; mtahurumiwa na Mwenyezi Mungu kutoka juu ya mbingu yake ya saba.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Dini ya Uislamu ni dini ya huruma, na dini nzima imesimama katika kumtii Mwenyezi Mungu na kuwatendea wema viumbe.
  • Mwenyezi Mungu aliyetakasika na kutukuka anasifika kwa sifa ya huruma, naye Mtukufu ni Mwingi wa rehema mwenye kurehemu, mfikishaji wa huruma kwa waja wake.
  • Malipo huendana na matendo, wenye huruma huwahurumia Rahman -Mwingi wa rehema-.