Anahimiza Mtume rehema na amani ziwe juu yake Maswahaba kufanya amali njema, na wamche Mwenyezi Mungu kadiri wawezavyo, pasina kuchupa mipaka wala uzembe, na wakusudie katika amali zao kupatia kwa kuwa na ikhlasi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kufuata mafundisho ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake ili amali zao zikubaliwe, ili iwe ni sababu ya kuteremka kwa rehema juu yao. Kisha akawaeleza kuwa amali hazitomuokoa yeyote miongoni mwao kamwe; bali ni lazima kuwe na rehema ya Mwenyezi Mungu. Wakasema: Hata wewe ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu hazitokuokoa amali zako pamoja na ukubwa wa kiwango chake? Akasema: Hata mimi, ila kama atanisitiri Mwenyezi Mungu kwa fadhila na rehema zake.