Anatoa habari Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa miongoni mwa alama kubwa za Kiyama, ni kuchomoza jua kutoka upande wa Magharibi badala ya upande wa Mashariki, na watu wakiliona wataamini wote, Na wakati huo haitomfaa kafiri imani yake, wala hayatomfaa matendo mema wala kutubia. Kisha akatoa habari Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Kiyama kitatokea ghafla; Kitatokea na watu watakuwa kwenye hali walizokuwa nazo na wapo kwenye mambo yao ya kimaisha; Na kitasimama Kiyama hali ya kuwa muuzaji na mnunuzi wamesambaza nguo zao lakini hawataweza kuuziana wala hawataweza kuzikunja. Na kitasimama Kiyama na hali ya kuwa mtu ameshika maziwa aliyoyakamua kutoka kwa Ngamia wake na wala hatoweza kuyanywa. Na kitasimama Kiyama na mtu atakuwa anatengeneza josho la kunyweshezea wanyama na kulisiriba na wala hatowahi kunywesheleza humo. Na kitasimama Kiyama na mtu atakuwa kainua tonge lake ili kulipeleka kinywani mwake ili ale na wala hatoweza kulila tonge hilo.