Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa watatokea watu katika zama za mwisho katika umma wake wakizua uongo, na wakisema mambo ambayo hakuyasema yeyote kabla yao, wataeleza simulizi za uongo na za kutunga, akatuamrisha -Rehema na amani ziwe juu yake- tujiweke mbali nao na wala tusikae nao, na wala tusisikilize mazungumzo yao; ili hadithi hizo za kutunga tusiziweke ndani ya nafsi, tukashindwa kujiepusha nazo.