Anaamrisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuifikisha elimu kutoka kwake katika Qur'ani na mafundisho yake (Sunna), hata kama kitu kitakuwa kidogo kama aya moja toka ndani ya Qur'ani au hadithi, kwa sharti mfikishaji awe mjuzi katika kile anachokifikisha na kuwalingania watu kwacho. Kisha akaweka wazi -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa hakuna ubaya kusimulia kuhusu wana wa Israeli kwa yale yaliyotokea kwao katika matukio, yale yasiyokinzana na sheria yetu. Kisha akatahadharisha kumzulia uongo, nakuwa yeyote mwenye kumzulia uongo kwa makusudi basi ajiandalie mwenyewe makazi yake motoni.