explain-icon

Ufafanuzi

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayemsemea uongo kwa makusudi kwa kumnasibishia kauli au kitendo kwa uongo, basi atambue kuwa Akhera atakua na makazi motoni; ndio malipo yake kwa kumsingizia kwake uongo.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Kumsemea uongo Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa makusudi kabisa ni sababu ya kuingia motoni.
  • Kumsemea uongo Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- si sawa na kuwasemea uongo watu wengine, kwa kuwa hilo linaambatana na madhara makubwa katika dini na dunia.
  • Hii ni tahadhari ya kusambaza hadithi kabla ya kuthibitisha usahihi wake kuwa ni kweli zimenasibishwa kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- au la!.