Alipita Hisham bin Hakim bin Hizam radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao, kwa wakulima wasiokuwa Waarabu huko Sham, wakiwa wamesimamishwa chini ya joto la Jua, akauliza kuhusu jambo lililowapata? Akaambiwa kuwa wamefanywa hivyo kwa sababu ya kutolipa Jizia (kodi) hali yakuwa wanauwezo wa kulipa. Amesema Hisham radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: Ninashuhudia kuwa hakika nilimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: Hakika Mwenyezi Mungu huwaadhibu wale wanaowaadhibu watu duniani kwa dhuluma pasina haki.