Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Ibilisi amekwishakata tamaa waumini wenye kuswali kurudi kuabudu na kusujudia masanamu katika kisiwa Arab, lakini bado anatamaa, na bado nguvu zake na juhudi zake na harakati zake ziko katika kuwachochea baina yao kwa ugomvi na chuki na vita na fitina na mfano wa hayo.