explain-icon

Ufafanuzi

Anakataza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kupitiliza na kuvuka mpaka wa kisheria katika kumsifu, na kumsifu kwa sifa za Mwenyezi Mungu Mtukufu na matendo yake ambayo ni yake pekee, au kusema kuwa anajua mambo yaliyo jificha, au anastahiki kuombwa pamoja na Mwenyezi Mungu, kama walivyofanya Wakristo kwa Issa mwana wa Mariam -Amani iwe juu yake- Kisha akaweka wazi kuwa yeye ni mja wa Mwenyezi Mungu, na akaamrisha tuseme kuhusu yeye: Mja wa Mwenyezi Mungu na Mjumbe wake.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Tahadhari ya kuvuka mpaka wa kisheria katika kuzikuza sifa; kwani hilo hupelekea katika ushirikina.
  • Aliyoyatahadharisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- tayari yamekwisha tokea katika umma huu, kundi likachupa mipaka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na kundi kwa watu wa nyumba yake, na kundi kwa mawalii wake (wacha Mungu), wakatumbukia katika ushirikina.
  • Amejisifu Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa yeye ni mja wa Mwenyezi Mungu; ili aweke wazi kuwa yeye ni mja anaelelewa na Mwenyezi Mungu haifai kuelekezewa chochote katika mambo mahususi ya kiuungu.
  • Amejisifu Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa yeye ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu; ili aweke wazi kuwa yeye katumwa kutoka kwa Allah hivyo, ni wajibu kumsadikisha na kumfuata.