explain-icon

Ufafanuzi

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu kufeli na kupata hasara kwa watiao ugumu -pasina uongofu wala kuwa na elimu- katika dini yao na dunia yao, na katika kauli zao na matendo yao, wenye kuvuka mipaka ya sheria aliyokuja nayo Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Uharamu wa misimamo mikali katika mambo yote, na himizo la kuepuka hilo katika kila kitu; hasa hasa katika ibada na kuwatukuza watu wema.
  • Kutafuta ukamilifu katika ibada na mengine mazuri; na kunakuwa kwa kufuata sheria.
  • Inapendeza kulitilia mkazo jambo muhimu, kwa sababu Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alikariri sentensi hii mara tatu.
  • Upole wa uislamu na wepesi wake.