Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa kuambukizana ambako walikuwa wakiamini watu wa zama za ujinga kuwa maradhi yanahama yenyewe kwenda kwa mwingine pasina kadari ya Mwenyezi Mungu, nikuwa madai hayo ni batili, nakuwa mikosi ya ndege ni batili, nayo ni mikosi kupitia kitu chochote chenye kuhisika au kuonekana, kama ndege au wanyama, au walemavu, au namba au siku au kinginecho, hapa ametaja ndege kwa sababu ni kitendo kilichokuwa maarufu zama za ujinga, na asili yake ilikuwa ni kumuachia ndege wakati wa kuanza kazi yoyote, kama safari au biashara au kinginecho, akiruka kuelekea kushoto mtu anaamini ni mkosi, na anaahirisha alichotaka kukifanya. Kisha akaeleza -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa anafurahishwa sana na mtu kujipa matumaini, nayo ni mtu kuwa na furaha na raha, kwa maneno mazuri anayoyasikia, yatakayomfanya awe na dhana nzuri na Mola wake Mlezi.