Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayekufa na akakutana na Mwenyezi Mungu akiwa na tauhidi hamshirikishi na chochote basi huyo ni katika watu wa Peponi, hata kama akiadhibiwa kwa dhambi motoni, na atakayekufa huku akimshirikisha Mwenyezi Mungu na chochote hakuna jema lolote litakalomnufaisha; na Pepo kwake ni haramu.