Alikuja mtu mmoja kwa Mtume rehema na amani zimfikie akamsemesha kuhusu jambo lake binafsi, kisha akasema: "Akitaka Mwenyezi Mungu na ukataka wewe", Mtume rehema na amani zimfikie akaikemea kauli hii, na akamueleza kuwa kuunganisha matashi ya kiumbe na matashi ya Mwenyezi Mungu kwa kiunganishi "na" ni shirki ndogo, haifai kwa muislamu kuitamka, kisha akamuelekeza katika kauli ya sawa na ya haki: "Akitaka Mwenyezi Mungu peke yake", ampwekeshe Mwenyezi Mungu katika matashi, na wala asiunganishe matashi ya yeyote kwa aina yoyote ya kiunganishi.