Alitoka Mtume rehema na amani zimfikie kwenda Hunaini: Nalo ni bonde liko kati Twaif na Makka, na walikuwa pamoja naye baadhi ya Masahaba waliokuwa hawana muda mrefu tangu kuingia ndani ya Uislamu, wakapita katika mti ukiitwa: "Dhaata anwaatwi", yaani: Wenye vifaa vya kutundikia, washirikina walikuwa wakiutukuza na wakitundika hapo silaha zao na vitu vingine kwa kutaka baraka, wakaomba kutoka kwa Mtume rehema na amani zimfikie awawekee mti mfano wake, wakitundika hapo silaha zao, kwa kutafuta baraka, kwa kudhani kwao kuwa jambo hilo linafaa, Mtume rehema na amani zimfikie akamtukuza Mwenyezi Mungu kwa kukemea kauli hiyo, na kwa kumtakasa Mwenyezi Mungu, na akawaeleza kuwa kauli hii inafanana na kauli ya watu wa Mussa kwake: "Tuwekee nasi mungu kama ambavyo wao walivyo na mungu", walipowaona wenye kuabudu masanamu wakaomba nao wawe na masanamu kama washirikina walivyo na masanamu, nakuwa kitendo hiki ni katika kufuata njia yao, kisha akaeleza Mtume rehema na amani zimfikie kuwa Umma huu utafuata mfumo wa Mayahudi na Wakristo na utafanya vitendo vyao, na akatahadharisha hilo.