Amesimulia mama wa waumini mama Salama radhi za Allah ziwe juu yake kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakwamba alipokuwa katika ardhi ya Ethiopia aliona Kanisa -linaloitwa kwa jina la Mtakatifu Maria- ndani yake kukiwa na picha na mapambo na michoro; akastaajabu kwa kitendo hicho!. Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akafafanua sababu za kuwekwa picha hizo; Akasema: Hakika hao unaowataja hapa walikuwa anapokufa kwao mtu mwema wanajenga Msikiti juu ya kaburi lake, na wanasali ndani yake, na wanachoro picha hizo, Na akabainisha kuwa mfanyaji wa hilo ni kiumbe muovu zaidi kuliko wote mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu; kwa sababu kitendo chake hicho kinapelekea katika kumshirikisha Mwenyezi Mungu Mtukufu.