explain-icon

Ufafanuzi

Othman bin Affan alitaka kuujenga msikiti wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa sura nzuri zaidi kuliko jengo lake la awali, watu hawakupendezwa na swala hilo; kwa sababu msikiti utabadilika kutoka katika muonekano wa jengo lake lilivyokuwa katika zama za Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, msikiti ulikuwa umejengwa kwa matofali, na paa lake lilikuwa limeezekwa kwa makuti, lakini Othman alitaka kuujenga kwa mawe na chokaa, Othman radhi za Allah ziwe juu yake akawaeleza kuwa yeye alimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: Atakayejenga msikiti kwa kutafuta radhi zake Mtukufu, si kwa kutaka kujionyesha au kusikika, Mwenyezi Mungu atamlipa malipo bora kulingana na amali yake, na malipo hayo ni Mwenezi Mungu kumjengea mfano wake peponi.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Himizo la kujenga misikiti na fadhila zake.
  • Kupanua msikiti na kuukarabati yote haya yanaingia katika fadhila za kujenga.
  • Umuhimu wa kutakasa nia kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.