Amemkataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake msimamizi wa mwanamke na muhusika wake kuwakataza wanawake kwenda Msikitini, na akawaamrisha wanawake wakati wa kutoka kwenda Msikitini watoke bila kujipuliza manukato na wasitoke kwa kujiachia kwa mapambo; ili wasiwe sababu ya fitina kwa wanaume.