Na miongoni mwa sunna za Mtume rehema na amani ziwe juu yake ni kuwa anaposwali Alfajiri anakaa katika mswala wake mpaka Jua linachomoza kwa kunyanyuka, na alikuwa hasimami kutoka katika mswala wake aliouswalia Alfajiri, mpaka Jua lichomoze. Jua linapochomoza anasimama, na walikuwa wakizungumza wanachukua katika baadhi ya mambo yao ya kabla ya Uislamu na huku yeye kanyamaza, wanacheka, na huenda yeye akatabasamu pamoja nao.