explain-icon

Ufafanuzi

Amemhimiza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- mwenye kuja msikitini na akaingia katika wakati wowote, na kwa lengo lolote, asali rakaa mbili kabla hajakaa, nazo ni rakaa mbili za salamu ya msikiti.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Sunna ya swala ya rakaa mbili kwa ajili ya salamu ya msikiti kabla ya kukaa.
  • Amri hii ni kwa atakayetaka kukaa, atakayeingia msikitini na akatoka kabla ya kukaa, amri hii haimuhusu.
  • Atakapoingia mwenye kuswali na watu wakiwa ndani ya swala, akaingia nao, basi hilo litamtosheleza na rakaa mbili.