explain-icon

Ufafanuzi

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa sehemu zinazopendeka zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni misikiti yake; kwa sababu ni nyumba za ibada, na zimeasisiwa kwa uchamungu, na miji inayochukiza zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni masoko yake; kwa sababu masoko mara nyingi ndio kitovu cha ghushi na udanganyifu na riba na viapo vya uongo, na kwenda kinyume na ahadi, na kupuuza kumtaja Mwenyezi Mungu.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Utukufu wa misikiti na heshima yake; kwa sababu ni nyumba ambazo hutajwa ndani yake jina la Mwenyezi Mungu kwa wingi.
  • Himizo la kudumu kuwa msikitini, na wingi kwenda ndani yake, kwa kutafuta mapenzi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na radhi zake, na kupunguza kuzunguka masokoni, isipokuwa kwa haja maalumu; kwa kujiepusha kuingia katika sababu za hasira ya Mwenyezi Mungu.
  • Amesema Nawawi: Misikiti ni mahali pa kushuka rehema na masoko ni kinyume chake.