Alieleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa matendo yapo aina sita, na watu wamegawanyika katika makundi manne, nayo ni: Kundi la kwanza: Yeyote atakaye kufa na hakumshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu chochote anastahiki kuingia peponi. Kundi la pili: Yeyote atakaye kufa hali yakuwa anamshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu kingine anastahiki kuingia motoni na atakaa humo milele. Na matendo hayo mawili ndiyo haki mbili za msingi. Kundi la tatu: Kukusudia kufanya wema, basi yeyote atakaye kusudia kufanya jema na akawa mkweli katika makusudio yake mpaka akahisi kweye moyo wake kuwa hili ndilo kusudio langu, kisha likamtokea jambo la kumzuia asifanye alichokikusudia katika wema huu, basi huandikiwa thawabu za wema kamili. Kundi la nne: Kufanya tendo baya; Yeyote atakaye fanya tendo baya basi huandikiwa kosa moja. Na matendo hayo mawili: Ndiyo hulipwa sawa sawa bila ya kuzidisha. Kundi la Tano: Jema moja hulipwa kwa kumi mfano wake, na malipo hayo ni kwa mwenye kukusudia kufanya wema na akaufanya wema huo, basi huandikiwa mema kumi. kundi la sita: Jema moja hulipwa sawa na mema mia saba, na malipo hayo ni kwa mwenye kutoa kitu kimoja katika njia ya Mwenyezi Mungu, basi hulipwa kwa kitu hiki kimoja kwa mema mia saba, na haya ni kutokana na fadhila za Mwenyezi Mungu aliyetakasika na Kutukuka, na ukarimu wake kwa waja wake. Ama aina Nne ya watu ni hawa: Aina ya kwanza: Ni mtu ambaye amekunjuliwa mambo yake hapa Duniani kwa upande wa riziki, ananeemeka humo na hupata akitakacho, lakini ni mwenye dhiki na tabu kubwa Akhera na mwisho wake ni kuingia motoni, na huyo ni tajiri wa kikafiri. Aina ya pili: Ni mtu mwenye dhiki hapa Duniani upande wa riziki, lakini amekunjuliwa huko Akhera, na mwisho wake ni kuingia Motoni, na huyo ni muumini fakiri. Aina ya tatu: Ni mtu mwenye dhiki hapa Duniani na Akhera, naye ni kafiri fukara. Aina ya nne: Ni mtu aliyekunjuliwa mambo yake hapa Duniani na Akhera, naye ni muumini tajiri.