Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alimtaka Abuu Twalib ambaye ni baba yake mdogo akiwa katika kilevi cha mauti, atamke neno Laa ilaaha illa llahu, ili amuombee utetezi kwa neno hilo siku ya Kiyama, na amtolee ushuhuda wa kusilimu kwake, akakataa kutamka shahada kwa kuogopea kuwa Makuraishi watamtukana na watamsema kuwa: Amesilimu kwa sababu ya kuogopa mauti na unyonge! Akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Kama si huko kuogopa ningeingiza furaha katika moyo wako kwa kutamka kwako shahada na mauti yangekufika kwa namna ambayo ungeiridhia! basi akateremsha Mwenyei Mungu Aya ambayo inajulisha kuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- hamiliki uongofu wa kuukubali uislamu, bali Mwenyezi Mungu aliyetukuka peke yake humuwezesha amtakaye. Na kuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake anawaongoza viumbe kwa ufahamu na kuwawekea wazi na kuwaongoza pamoja na kuwaita kwenye njia iliyonyooka.