Alisema bin Abbasi Mwenyezi Mungu amuwie radhi kumwambia Atwaa bin Abii Rabaahi: Je, nikuonyeshe mwanamke miongoni mwa watu wa Peponi? Atwaa akasema: Ndio, akasema: Huyu mwanamke muethiopia mweusi, alikuja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake: akasema: Hakika mimi nina maradhi, huanguka na kufunuka nguo zangu, na kuonekana sehemu ya mwili wangu pasina mimi kujielewa, basi muombe Mwenyezi Mungu aniponye, akasema: Ukipenda unaweza kuvumilia na utakuwa na malipo ya Pepo, na ukipenda nitamuomba Mwenyezi Mungu akuponye, akasema: Basi nitavumilia, kisha akasema: Basi niombee kwa Mwenyezi Mungu nisifunuke nikianguka, basi akamuombea kwa Mwenyezi Mungu.