Aliingia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa Ami yake Abuu Twalib akiwa katika hali ya kukaribia kufa, akasema kumwambia: Ewe Ami yangu sema "Laa ilaaha illa llaah", neno ambalo nitakutolea ushahidi kwalo mbele ya Allah, Abuu Jahali na Abdallah Bin Abiiy Umaiyya wakasema: "Wewe Abuu Twalib!, unaacha mila ya baba yako Abdul Muttwalib?! ambayo ni kuabudu masanamu, wakaendelea kumwambia hivyo mpaka akasema neno lake la mwisho alilowaambia kuwa: Niko katika mila ya Abdul Muttwalib, mila ya ushirikina na kuabudu masanamu, Akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Nitakuombea msamaha madam sijakatazwa na Mola wangu kuhusu hilo, ikateremka kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Haipasi kwa Nabii na wale walioamini kuwatakia msamaha washirikina, hata kama watakuwa ni jamaa zao, baada ya kwisha bainika kuwa hao ni watu wa Motoni" [Attauba: 113], Na ikateremka kumuhusu Abuu Twalib kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Hakika wewe, humuongoi, unayependa aongoke. Lakini Mwenyezi Mungu, Anamuongoa Anayemtaka. Na Yeye Ndiye Anayemjua zaidi anayefaa kuongoka". Kwani hakika wewe humuongoi umpendaye kumuongoa, bali jukumu lako ni kufikisha, na Allah anamuongoa amtakaye.