Anatoa habari Anas Bin Maalik -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Wakati mmoja Maswahaba walikuwa wamekaa pamoja na Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Msikitini aliingia mtu mmoja akiwa juu ya Ngamia, basi akampigisha magoti kisha akamfunga Ngamia wake, Kisha akawauliza: Kati yenu Muhammad ni nani? Na Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa amekaa kati ya watu na ameegemea, tukamwambia: Ni mtu huyu mweupe aliyeegemea, Yule bwana akamwambia: Ewe mtoto wa Abdul Muttwalib, Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Nimekusikia, basi uliza nitakujibu. Yule bwana akamwambia Mtume -Rehema na mani ziwe juu yake-: Mimi nitakuuliza na nitakuuliza kwa msisitizo mkubwa hivyo usinichukie wala usione dhiki katika nafsi yako. Yaani: Usinikasirikie wala usione dhiki, Akasema: Uliza unachotaka, Akasema: Ninakuuliza kwa jina la Mola wako na Mola wa waliokuwa kabla yako, Je ni kweli Mwenyezi Mungu amekutuma kwa watu wote? Akasema: Ndiyo ni kweli, hali ya kutilia mkazo ukweli wake, Yule bwana akasema: Ninakuuliza kwa jina la Mwenyezi Mungu, je ni kweli Mwenyezi Mungu amekuamrisha yakuwa sisi tusali sala tano usiku na mchana? Nazo ni sala za faradhi, Akasema: Ndiyo ni kweli, Akasema: Ninakuuliza kwa jina la Mwenyezi Mungu, je ni kweli Mwenyezi Mungu amekuamrisha yakuwa sisi tuufunge Mwezi huu katika kila Mwaka? Yaani Mwezi wa Ramadhan, Akasema: Ndiyo ni kweli, Akasema: Ninakuuliza kwa jina la Mwenyezi Mungu, je ni kweli Mwenyezi Mungu amekuamrisha kuwa uchukue hizi sadaka kutoka kwa matajiri wetu kisha uzigawe kwa mafukara wetu? Na sadaka hiyo ni Zaka, Basi akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-Ndiyo ni kweli, Basi Dhwamamu akasilimu, na akamwambia Mtume-Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa yeye atawalingania watu wake kuingia kwenye uislamu, kisha akajitambulisha kuwa yeye ni Dhwammam Bin Thaalabah atokanae na kabila la Banii Saad Bin Bakri.