Ulikuwa usia mwingi wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa Umma wake naye akiwa katika ulevi wa kifo: Shikamaneni na swala na mdumu nayo na wala msighafilike nayo, na vile vile timizeni haki za wale wanaomilikiwa na mikono yenu ya kuume miongoni mwa watumwa na wajakazi na wamilikini kwa wema, akaendelea kuukariri, mpaka ukaanza kumkwama katika koo lake, na ulimi wake ukashindwa kuutamka kwa ufasaha.