explain-icon

Ufafanuzi

Amebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa baba awaamrishe watoto wake wa kiume na wa kike kusali na umri wao ukiwa mikaa saba, na awafundishe wanayoyahitaji kwa ajili ya kuitekeleza. Na wakifikisha miaka kumi azidi kutilia mkazo, awapige wanapofanya uzembe, na awatenganishe katika vitanda.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Kuwafundisha dini watoto wadogo kabla hawajabalehe, na hasa hasa swala.
  • Kipigo kinakuwa ni kwa ajili kutia adabu, nasi kwa kuadhibu, apige kipigo kinachoendana na hali yake.
  • Sheria imetilia umuhimu kuhifadhi heshima, na kuziba kila njia inayopelekea kuiharibu.