Anaeleza bin Abbasi -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- aliwafundisha hotuba ya haja (dharura), nayo ni ile inayosemwa wakati wa kufungua mazungumzo katika hotuba na wakati wa shida zao, kama hotuba ya ndoa na hotuba ya Ijumaa na nyinginezo, Na hotuba hii imekusanya maana tukufu, kwanzia kubainisha ustahiki wa Mwenyezi Mungu wa aina zote za kuhimidiwa, na kutaka msaada kutoka kwake yeye pekee asiye na mshirika wake, na stara ya madhambi na kusamehewa, na kuomba kinga kwake dhidi ya kila shari, na shari za nafsi na nyinginezo. Kisha akaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa uongofu uko mkononi mwa Mwenyezi Mungu, mwenye kumuongoza hakuna wa kumpoteza, na anayempoteza hana wa kumuongoza. Kisha akataja shahada ya tauhidi nakuwa hakuna muabudiwa wa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, na shahada ya ujumbe kuwa Muhammadi ni mja wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na ikahitimisha hotuba hii kwa aya hizi tatu zilizojaa amri ya kumcha Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kufanya maamrisho yake na kuyaepuka makatazo yake kwa kutaka radhi za Mwenyezi Mungu, nakuwa malipo ya mwenye kufanya hivyo ni kutengemaa kwa matendo na kauli, na kusamehewa madhambi na kufutwa makosa na maisha mazuri duniani na kufaulu kwa kuipata pepo siku ya Kiyama.