explain-icon

Ufafanuzi

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu mambo mawili nayo muislamu basi ataingia Peponi, La kwanza: Kuhifadhi ulimi kutozungumza yale yenye kumchukiza Allah Mtukufu, La pili: Kuhifadhi tupu kutotumbukia katika machafu; Kwa sababu viungo viwili hivi hukithiri kutokea maasi kwavyo.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Kuhifadhi ulimi na tupu ni njia ya kuingia Peponi.
  • Umetajwa mahususi ulimi na utupu; kwa sababu ndio vyanzo vikuu vya balaa kwa mwanadamu katika dunia na Akhera.