Walikuja baadhi ya watu kwa mmoja kati ya Masahaba wakimuuliza kuhusu Mimbari ya Mtume aliyoitumia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Ilitengenezwa kwa kitu gani? Na walikuwa wamekwisha bishana na kuzozana katika hilo, akawaeleza kuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-aliagiza kwa mwanamke wa ki Answari alikuwa na mtumishi seremala, akamwambia: Mwamrishe kijana wako anitengenezee Mimbari nikalie wakati nikizungumza na watu, mama yule akakubali ombi hilo, na akamuamrisha kijana wake amtengeneze Mimbari Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kutokana na mti wa Twarfaa (Mti mfano wa mkaratusi), kijana alipomaliza kazi, yule mama aliaigiza kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Mtume akaamrisha iwekwe mahala pake msikitini, kisha akaswali Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akiwa juu yake, na akatoa takbira akiwa juu yake, kisha akarukuu akiwa juu yake, kisha akashuka akiwa anatembea kwa nyuma bila ya kugeuka kutazama nyuma, akasujudu mwishoni mwa Mimbari, kisha akarudi, alipomaliza swala akawageukia watu, na akasema: Enyi watu!, Bila shaka nimefanya hivi ili muige na mjifunze swala yangu.