Anaeleza Mtume Rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakaposwali muislamu katika jamaa, swala yake hiyo itakuwa bora kuliko swala yake nyumbani kwake au sokoni kwake kwa zaidi ya mara ishirini. Kisha akaeleza sababu ya hilo: Nayo nikuwa mtu atakapotawadha akatimiza vizuri udhu na ukaufanya vizuri, kisha akatoka kwenda Msikitini hakuna kinachomtoa ila kukusudia kusali, hatopiga hatua yoyote isipokuwa atanyanyuliwa kwa hatua hiyo daraja na nafasi ya juu, na hufutiwa kwake kwa hatua hiyo makosa, Atakapoingia Msikitini na akakaa akisubiri swala, basi atapata malipo ya swala na thawabu zake kwa muda wote atakaokaa akisubiri swala, na Malaika wakimuombea akiwa katika kikao chake aliposwalia, wakisema: "Ewe Mwenyezi Mungu msamehe, ewe Mwenyezi Mungu muhurumie, ewe Mwenyezi Mungu mfutie makosa" Huendelea kumuombea madam hajaharibu udhu wake, au akafanya yanayowakera watu au Malaika.