explain-icon

Ufafanuzi

Mtume rehema na amani ziwe juu yake amemkataza atakayekuwa msikitini aanze kuswali sunna baada ya kukimiwa swala ya faradhi.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Katazo la kuswali sala ya sunna itakapokimiwa swala ya faradhi msikitini.
  • Katazo la kuanza sunna baada ya kukimiwa swala, sawa sawa iwe ni sunna yenye utaratibu maalumu kama sunna ya Alfajiri na Adhuhuri au nyingineyo.
  • Pindi itakapokimiwa swala akiwa ndani ya sala ya sunna; ikiwa amebakiza kiasi kidogo chini ya rakaa moja basi ataikamilisha kwa haraka, na isipowezekana basi ataikatisha ili aipate takbira ya kuanza swala.