Alikuwa Muadhi bin Jabali -Radhi za Allah ziwe juu yake- amepanda nyuma ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- juu ya mnyama wake, akamuita: Ewe Muadhi? Akarudia wito mara tatu; Kwa kusisitiza umuhimu wa yale atakayomueleza. Na mara zote hizo Muadhi -Radhi za Allah ziwe juu yake- akimjibu kwa kusema: "Labaika kwa heshima yako ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu", Yaani: Nimekujibu ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu jibu moja moja, na ninataka utukufu kwa kukujibu wewe. Akaeleza -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa hakuna yeyote atakayeshuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuaubudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, Yaani: Hakuna muabudiwa wa haki isopokuwa Allah, na kuwa Muhammadi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, kwa ukweli toka moyoni mwake, si muongo, ikiwa atakufa katika hali hii basi Mwenyezi Mungu atamharamisha kuingia motoni. Muadhi -Radhi za Allah ziwe juu yake- akamuomba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- awaeleze watu ili wafurahi na wajipe bishara njema? Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akachelea watu kubweteka katika hilo, na wapunguze kufanya matendo. Muadhi hakumsimulia hilo yeyote ila kabla ya kifo chake; kwa kuhofia kuingia katika dhambi za kuficha elimu.