Aliulizwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu dhambi kubwa akasema: Kubwa zaidi ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu, nako ni kumuwekea Mwenyezi Mungu mfano katika uungu wake au uumbaji wake au majina yake na sifa zake, na dhambi hili halisamehe Mwenyezi Mungu isipokuwa kwa toba, na akifa mfanyaji wake huyo atakaa milele motoni. Kisha ni mtu kumuua mwanaye kwa kuchelea kula naye, na kuua nafsi ni haramu, lakini dhambi linakuwa kubwa pale anapokuwa muuliwaji ni ndugu wa damu wa muuaji, na dhambi lake linakuwa kubwa pia pale linapokuwa lengo la muuaji ni kuchelea kushirikiana pamoja na muuliwaji katika riziki ya Mwenyezi Mungu. Kisha ni mtu kumzini mke wa jirani yake kwa kujaribu kumhadaa mke wa jirani yake mpaka akafikia kuzini naye, naye akamkubalia, Na zinaa ni haramu lakini dhambi lake linakuwa kubwa anapokuwa mziniwa ni mke wa jirani ambaye sheria imeusia kumtendea wema na kuishi naye vizuri.