Anatueleza Ally bin Husein -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba yeye alimuona mtu mmoja akimuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kaburi la Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-, nakuwa yeye alimkataza juu ya hilo kwa ushahidi wa hadithi ya Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- ambayo limekuja ndani yake katazo la kulifanyia mazoea kaburi lake kwa ziara, na katazo la kuzitelekeza nyumba kwa kutokuwa na ibada ya Mwenyezi Mungu ndani yake na dhikri, na kuifananisha kwake na kaburi, na akaeleza kuwa salamu ya muislamu itamfikia yeye -Rehema na Amani ziwe juu yake- mahala popote atakapokuwa muislamu.