Walikuja watu miongoni mwa washirikina kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na walikuwa wamekwisha fanya mauaji mengi na zinaa nyingi, wakasema kumwambia Mtume: Hakika Uislamu unaoulingania na mafundisho yake ni mazuri, lakini sisi tutakuwa na hali gani kwa yale tuliyoyatenda miongoni mwa ushirikina na madhambi makubwa, je, yanakafara?. Zikateremka aya mbili, kiasi ambacho Mwenyezi Mungu aliwakubalia watu toba zao pamoja na wingi wa madhambi yao na ukubwa wake, na lau kama si hivyo basi wangeendelea kubaki katika ukafiri wao na ujeuri wao wala wasingeingia katika dini hii.