explain-icon

Ufafanuzi

Anaeleza Mtume Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu tiba sahihi ya kujiepusha na maswali ambayo Shetani huyatumia kumtia wasiwasi muumini, Basi Shetani husema: Ni nani aliyeumba kitu fulani? Ni nani aliyeumba mbingu? Ni nani aliyeumba Ardhi? Hivyo basi muumini kutokana na dini yake na maumbile yake na akili yake humjibu kwa kusema kuwa ni Mwenyezi Mungu, Lakini Shetani haishii hapo kwenye kutia wasiwasi, bali anahama mpaka anafikia kusema; Ni nani aliyemuumba Mola wako? Basi wakati huo muislamu atajizuilia na wasiwasi huu kwa kufanya mambo matatu: Kwa kumuamini Mwenyezi Mungu. Na kwa kujikinga kwa Mwenyezi Mungu kutokana na Shetani, Na kuacha kuendekeza wasiwasi.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Kupinga wasiwasi wa Shetani na hatari zake na kuacha kufikiria wasiwasi, na kukimbilia kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kuondosha wasiwasi.
  • Kila aina ya wasiwasi unaotokea kwenye moyo wa mwanadamu na unapingana na sheria basi wasiwasi huo ni wa Shetani.
  • Kumekatazwa kufikiria dhati ya Mwenyezi Mungu, na kuhimizwa kufikiria kuhusu viumbe wa Mwenyezi Mungu na alama zake.