Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa tutatawaliwa na viongozi ambao tutayajua baadhi ya matendo yao kuwa yako sawa na yale yanayofahamika ndani ya sheria; na tutayakemea baadhi yake kwa kuwa kwake kinyume na sheria, Atakayechukia moyoni mwake na akawa hakuweza kukemea; basi atakuwa kaondoa dhima ya kupata dhambi na unafiki, Na atakayeweza kukemea kwa mkono au ulimi akawakemea kwa hilo basi atakuwa kasalimika na maasi na kushiriki katika maasi, Lakini atakayeridhia matendo yao na akawafuata ataangamia kama walivyoangamia. Kisha wakamuuliza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Kwa nini tusiwapige vita viongozi ambao wanasifa kama hizi? Akawakataza wasifanye hivyo, na akasema: Hapana, msifanye hivyo madama wanasimamisha swala kwenu nyinyi.