Amebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayetoka katika kuwatii viongozi, na akaeneza fitina na kuusambaratisha umoja wa Uislamu uliokubaliana juu ya kumtii kiongozi, akafa katika hali hiyo ya faraka na kutomtii kiongozi, atakuwa kafa kifo cha watu wa zama za ujinga, ambao walikuwa hawamtii kiongozi yeyote wala hawajiungi katika kundi moja, bali walikuwa makundi makundi na wabaguzi, wakipigana wao kwa wao. Na akaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayepigana chini ya bendera ambayo haiko wazi upande wa haki au batili, anachukia kwa sababu ya ubaguzi wa watu wake au kabila lake, na si kwa kuitetea dini na haki, akapigana kwa ubaguzi pasina kuwa na ujuzi na elimu, akiuawa katika hali hiyo, atakuwa ni sawa na aliye uawa katika zama za ujinga. Nakuwa atakayetoka katika Umma wake -Rehema na amani ziwe juu yake- akimpiga mwema wake, na muovu wake, na wala hajali anayoyafanya na wala haogopi adhabu zake kwa kumuuwa muumini, na wala hawatendei uadilifu makafiri waliochukua ahadi au viongozi, bali anatengua ahadi kwao, jambo hili ni katika madhambi makubwa, atakayelifanya atakuwa amestahiki ahadi hii ya adhabu kali.