Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- anapokea sehemu katika sifa ya swala ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, na anaeleza kuwa alipokuwa akisimama katika sala anatoa takbira wakati ananyanyuka, nayo ni takbira ya kuhirimia swala, kisha anatoa takbira wakati anahama kwenda katika rukuu, na wakati anasujudu, na wakati anaponyanyua kichwa chake kutoka katika sijida, na wakati anasujudu sijida ya pili, na anaponyanyua kichwa chake kutoka katika sijida hiyo, na anaponyanyuka katika rakaa mbili za mwanzo baada ya kikao cha tashahudi ya kwanza katika swala yenye rakaa tatu au nne, kisha anafanya hivyo katika swala nzima mpaka anamaliza, na alikuwa akisema anaponyanyua mgongo wake kutoka katika rukuu: Sami'allaahu liman hamidah, kisha anasema akiwa wima: Rabbanaa lakal hamdu. Kisha anasema Abuu Huraira wakati anapomaliza swala: Namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hakika mimi swala yangu iko karibu zaidi kufanana na swala ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- zaidi yenu, bali hii ndio ilikuwa sifa ya sala yake mpaka alipoondoka duniani.