Ameeleza Omari radhi za Allah ziwe juu yake ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alisimama baada ya kumpopoa mawe Maaizi bin Malik Al-Aslami radhi za Allah ziwe juu yake, kwa adhabu ya zinaa, akawahutubia watu, na akasema: Jiepusheni na chafu hili na yote yanayotia kinyaa na machafu miongoni mwa maasi aliyoyakataza Mwenyezi Mungu, na atakayeangukia na akafanya chochote basi ni wajibu kwake mambo mawili: La kwanza: Ajifiche katika mahali alipomsitiri Mwenyezi Mungu, na asimueleze yeyote kuhusu maasi yake. La pili: Afanye haraka kutubia kwa Mwenyezi Mungu na wala asiendelee, na yatakayeonekana wazi maasi yake basi tutamsimamishia sheria iliyotajwa ndani ya kitabu cha Mwenyezi Mwenyezi kwa maasi hayo.