Ukba bin Aamiri alimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu sababu za muumini kuokoka katika dunia na Akhera? Akasema rehema na amani ziwe juu yake: Shikamana na mambo matatu: La kwanza: Hifadhi ulimi wako katika yale yasiyokuwa na kheri ndani yake, na kuzungumza kila shari, na usitamke ila la kheri. La pili: Baki nyumbani kwako ili umuabudu Mwenyezi Mungu katika nyakati za faragha, na ujishughulishe na kumtii Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa ibada, na jitenge nyumbani kwako na fitina. La tatu: Lia na ujute na utubie kwa yale uliyoyatenda katika madhambi.