Katika zama za Mtume rehema na amani ziwe juu yake kulikuwa na bwana mmoja jina lake Abdallah, na akiitwa Punda, kwa jina la utani, na alikuwa akimchekesha sana Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika baadhi ya maneno yake, na alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amekwisha mchapa kwa sababu ya kunywa pombe, siku moja akaletwa tena akiwa amekunywa pombe, akaamrisha akachapwa. Mmoja kati ya waliopo akamtukana, na akasema: Mwenyezi Mungu mlaani, amezidi sana kuletwa kwa sababu ya kunywa pombe?! Akasema rehema na amani ziwe juu yake: Msimuombee kufukuzwa katika rehema ya Mwenyezi Mungu, na Wallahi sijajua lolote kwake isipokuwa anampenda Mwenyezi Mungu na Mtume.