Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu siku ya Kiyama atakapowakusanya wa mwanzo na wa mwisho kwa ajili ya hesabu, atasimika kwa kila haini ambaye hakutimiza ahadi aliyokubaliana nayo kwa Mwenyezi Mungu au pamoja na watu, alama ambayo atamfedhehesha kwayo mbele za watu kwa sababu ya hiana yake, na kutanadiwa juu yake siku hiyo: Hii ndio hiana ya fulani bin fulani; kwa ajili ya kutangaza ubaya wa kitendo chake mbele ya waliokusanyika katika uwanja halaiki (mahashari).